Ben Pol amesema aliamua kumpa Nisher kazi ya kuongoza video yake ya
Jikubali kwakuwa alifahamu ni mtu aliyekuwa na hasira ya kuonesha uwezo
wake.
"Kikubwa niliona ni mtu ambaye ana moto, unajua mtu anapokuwa ameanza
halafu ana moto obvious anataka kufanya vitu vizuri vikubwa yaani damu
inachemka unaweza kusema anatafuta exposure pia," amesema Ben Pol
"Kwahiyo nilimpa kwa sababu hizo, kwa sababu niliona yeye kazi zake
za mwanzo alizozifanya za akina MABESTE za akina nani ni kazi kali sana.
Anafanya kwa nguvu sana na ubora wa hali ya juu.
Kwahiyo nikaona huyu mtu akipata audio nzuri anaweza kufanya kitu
kikubwa ndio maana nikafikiria kumpa. Nikaona bado ni mpya, bado ana
njaa, bado ana ubunifu mwingi, unajua tofauti na ukimpa director ambaye
ameridhika ana miaka mitano, kumi katika industry anaweza akakufanyia
kama moja ya kazi zake za kila siku kwa hiyo mimi nilikuwa naiepuka.
Kwahiyo mimi nilikuwa nataka kama mtu unampa kazi afanye kazi hiyo hiyo
pekee yake."
Source: Times Fm [the QUARTZ Blog]
Home
»
PRESS RELEASE
» UPDATE | Sababu za Ben Pol Kufanya Kazi na Director Nisher [Video ya JIKUBALI]
Tuesday, October 29, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.
![.](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqYouQ5f9yiXEsAyk7xGeEkgQHDFXrUqwnjXasZPcr07OlN06O8MQWpualUqtDth9R6FATZEQDTydeVGCPWKH19E2fBYDtQHtvJeywv-81lcfL8vwGp4aiPUyXjV8t9Nl4a0HCcpfoK62n/s640/Screen+shot+2012-11-21+at+5.59.57+PM.png)
0 comments:
Post a Comment